Tumefikia wapi katika kushirikisha vijana katika masuala ya uraia?

Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007, kijana Tanzania ni mtu mwenye umri wa kuanza miaka 15 hadi miaka 35. Na kwa mujibu  wa katiba ili kupiga kura mtanzania lazima awe na umri kuanzia miaka 18.

Suala la vijana kushiriki katika shughuli za kiraia kunajumiisha  vijana kutambua majukumu yao kama raia, kutambua nafasi za uongozi zilizo wazi kwa wao kuwania na kushiriki katika shughuli za kisiasa na maendeleo ya jamii zao kwa ujumla.

Takwimu zilizotolewa na utafiti uliofanywa na kituo cha Sheria na Haki za binadamu Tanzania (LHRC) na TACCEO kuhusu ufahamu wa kiraia wa vijana katika chaguzi zilizo pita za mwaka 2015-2020 zilionyesha kwamba 57% ya wahojiwa hawakuwahi kuhudhuria, kushiriki au kusikia taarifa za uwepo wa programu za kuchochea utambuzi wa kiraia kwa vijana.

Hali hii inatisha sana ukizingatia kwamba takriban 50% ya watanzania ni vijana na ndio wanategewa kufuatilia michakato ya uchaguzi kutokana na ufatiliaji mkubwa wa mitandao ya jamii, pia kushiriki na kuwania nafasi za uongozi

24% ya vijana katika utafiti huo waliripoti kutambua uwepo wa programu za namna hiyo na 19% tu walilipoti kushiriki kwenye programu za namna hiyo.

Moja wa kilimanjaro uliongoza kwa vijana walioshiriki kwenye program za utambuzi wa kisiasa kwa 67%, ikifuatiwa na mikoa ya Dar es salaam 63%, Tanga 59%,Tabora 39% na Kigoma 37%.

Ukiachana na uwekazo wa vijana kupewa ujuzi wa kuchanganua sera za siasa na kutambua majukumu na haki zao kama raia bado kunakikwazo kikubwa kwa vijana kushiriki katika kugombea nafasi za uongozi. Hii inatokana na kwamba vijana wengi sana sio wanachama wa vyama vya siasa, wengi hushikiria tu sera za chama fulani kisha kuibuka katika kampeni na mikutano pasipo kuchukua kadi za uwanachama.

Katika chaguzi za mwaka 2015-2020 kulikuwa na ongezeko la wabunge vijana ambapo wabunge 47 walichaguliwa wakiwa kati ya umri wa miaka 21 na 35.

Vijana wachache wanao miliki kadi ya chama wanaishia kuwa askari wa miguu wa wagombea watu wazima wakiwapeperushia bendera za kampeni pasipo kupewa nafasi za kushiriki katika maamuzi kwenye mikutano mikubwa ya vyama vyao.

Hali ngumu za kiuchumi kutokana na kukosa ajira na kipato duni vimechangia vijana kunasa kwenye chambo za zawadi ndogondogo na kushiriki kwenye kunakshi wagombea matajiri,  kuandamana na hata kufanya fujo.

Jambo lingine linalokwamisha ushiriki wa vijana katika shughuli za kiraia ni kutokuwa na motisha ya kushiriki katika mikutano ya ngazi za chini za kimaendeleo kuanzia mitaani, kwenye kata na hata wilayani. 

Serikali ya awamu ya 5 imeonyesha Miami mkubwa katika kuteua vijana katika nafasi za ukuu wa wilaya na ukuu wa mikoa jambo la kuleta faraja kubwa na motisha kwa vijana wengi. Tukielelea chaguzi za serikali ya awamu ya 6 mwaka 2020, tunayo nafasi kubwa ya kuelimisha vijana juu ya majukumu na haki zao za kiraia kwa kutumia mitandao ya jamii na semina mbalimbali. Kwa Kufanya huvi tutawawezesha vijana kushiriki kwa wingi na kwaukamirifu.swSwahili
en_USEnglish swSwahili