Ilani ya vijana: Sauti ya Vijana kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ilani ya vijana ni nini?

Ushirikishwaji wa kisiasa wa makundi yote ya kijamii sio tu haki ya msingi ya kisiasa na kidemokrasia pia ni msingi thabiti katika kujenga jamii zenye amani na kuunda sera zinazojibu mahitaji maalum ya vizazi vyote. Lakini, ingawa vijana ndio gurudumu la mabadiliko na wakombozi wa jamii zao na uchumi, uwanja wa siasa bado umetawaliwa na watu wazima. Ushiriki wa kiraia wa vijana hasa wenye umri wa miaka 18 hadi 25 unaendelea kuwa chini kuliko mikundi mengine yote katika jamii. Hali inayotisha ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kundi hili ni takriban 19% ya wakazi wote Tanzania.

Nguzo kuu ya uhamasishaji wa vijana ni vijana wenyewe, hii ni dhahiri ukizingatia vijana wameweza kuonyesha uwezo wa kujipanga, kuwasiliana, ushawishi na  nguvu ya kufanya mabadiliko. Namna mojawapo ya kuwajengea uwezo vijana wa kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe na pia kuwasilisha agenda yao serikalini ni kwa kuteengeneza Ilani ya vijana.

Ilani ni tamko rasmi la umma la dhamira, maoni, malengo, au nia ambazo zinaweza kutolewa na chama cha siasa, serikali, asasi za kiraia (AZAKI) au kikundi cha kijamii. Ilani mbalimbali hutengenezwa kabla ya uchaguzi mkuu Tanzania , zikiwemo ilani za vyama, asasi za kiraia, wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Harakati kwanza za kutengeneza ilani ya vijana ilianzishwa na asasi ya vijana ya Tanzania Youth Vision Association (TYVA) mwaka katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo waliweza kuandaa ajenda ya vijana. Mwaka 2015 asasi 8 za vijana ikiwemo shirika la “Restless Development”, Tanzania Youth Vision Association, (TYVA), FEMINA, Youth of United Nations Association (YUNA), Youth for Africa (YOA), TAMASHA and Zanzibar, Fighting Against Youth Challenges (ZAFAYCO). kwa umoja wao waliweza kuwasiliana na vijana kutoka mikoa 19 ya Tanzania kwa lengo la Kutambua ushiriki wa vijana katika uraia, maoni yao juu ya mipango ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa kwa kutambua vipaumbele 10 vya  maendeleo kwa katika miaka mitano ijayo.

Vipaumbele hivyo vinalengo la kuonyesha jukumu na ushawishi wa vijana sio tu katika kuchangia malengo ya maendeleo nchini Tanzania bali pia katika kiwango cha kimataifa. Ilikurahisisha ujumbe wa vijana kwa serikali, vyama vya siasa  na wagombea vipaumbele hivyo viliwekwa katika makudi yafuatayo;

  1. Ajira ya Vijana
  2. Elimu
  3. Huduma Bora za Afya
  4. Utawala Bora na Uwajibikaji
  5. Ushiriki wa Vijana na Ushiriki katika vyombo vya Kufanya Maamuzi
  6. Vijana na Maliasili, Michezo
  7.  Sanaa na Ubunifu
  8. Vijana wenye Ulemavu
  9. Usawa wa kijinsia  na,
  10.  Vijana na diplomasia.

“Ilani ya vijana inaweza kutumika katika kuwawajibisha viongozi walioteuliwa katika uchaguzi mkuu na kuhamasisha mabadiliko ya sera.  Ni ujumbe wenye lengo la kukusanya nguvu na kuhamasisha mabadiliko ya kiutawala. Ilani ya vijana inabeba mapendekezo ya vijana bungeni.”

Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi na kwa mara nyingine vijana wakitanzania wanahitaji kuwa na sauti moja. Ilani mpya ya vijana ya mwaka 2020 inahitaji kuhakisi mahitaji ya ustawi wa vijana wa ilikuhamasisha uundaji wa sera za maendeleo zinazohakikisha ukuaji wa pato la taifa, lakini pia kuboresha hali binafsi za kiuchumi za watanzania hasa vijana wenyewe ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Mwaka huu wa uchaguzi Umoja wa Asasi za vijana (Ajenda ya Vijana), utahakikisha vijana kitanzania wanashiriki kikamilifu kwenye shughuli katika uchaguzi kwa kuandaa ilani ya vijana ya mwaka 2020-2025. Ajenda ya Vijana itatoa vipaumbele vya kimaendeleo vinavyogusa mahitaji ya ya vijana wa kitanzania kwa kutoa fursa kwa vijana kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kushiriki kuamua juu ya mustakabali wa Tanzania kwa kuandaa Ilani ya vijana. Ilani hii ndio itakayo taarifu na kuongeza uelewa mzuri wa masuala ya vijana katika shughuri za maendeleo na kuwapa jukwaa la kupokea maoni yao juu ya masuala kadhaa muhimu.swSwahili
en_USEnglish swSwahili